REA yahimiza utumiaji majiko nishati safi

By Pilly Kigome , Nipashe
Published at 12:26 AM Jul 08 2025
Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy
Picha: Pilly Kigome
Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali pamoja na mkakati wa taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kujikita katika kusambaza majiko ya umeme, kufunga mifumo ya nishati safi ya kupikia kwenye Magereza.

Kuiwezesha Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi(VETA) kutengeneza mkaa mbadala ikiwemo na kusambaza majiko.banifu mijini na vijinini.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhanisi Hassan Saidy, katika Viwanja vya Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam maarufu Sabasaba.

Saidy amesema mikakati ya REA wanahakikisha maeneo ya  vijijini wanapata aina zote za nishati safi za kupikia, umeme ikiwemo na vituo vya mafuta vya magari.

Amesema tayari vijiji 12,318 vimeshafikiwa na huduma za umeme na serikali inaendeleza kupeleka umeme kwa kasi kubwa kwenye vitongoji vyote nchini kufikia malengo kila mtanzania atumie nishati hiyo.

Amesema hivi sasa agenda kubwa ya taifa ni nishati safi inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kuondoa upishi wa kizamani wa kiasili wa mafiga matatu kuondoa athari za mazingira zitokazo na nishati ambayo si salama kwa wananchi wote

Amefafanua malengo ya REA ifikapo 2034 angalau kuwe na asilimia 80 ambao tayari wamehama matumizi ambayo si salama wahamie kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia hususani wanawake.ambao wengi ndio wahanga katika.matumizi ambayo si sahihi.

Vilevile ametoa wito kwa watanzania waachane na dhana ya kudhani kuwa nishati safi inatumia gharama si sahihi na watumie nishati safi kuwa haina gharama kubwa.

"Tumeshaanza kuwawezesha wananchi vijijini matumizi ya nishati safi na tunaona tumeshafaulu kwa asilimia 20  kumeshawatoa wananchi kuachana na nishati ambayo sio salama ila kwa juhudi tunazofanya kutoa elimu tunaelekea kuwatoa kwa zaidi kubwa zaidi," amesema