Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabasi ya Mwendokasi (UDART), Waziri Kindamba amesema mwendokasi iligeuka kuwa mwendohasira na kwamba hatua zimechukuliwa mabasi mapya ya kisasa 99 yatawasili Julai,mwaka huu.
Aidha,amesema basi jipya la majaribio linalotumia gesi asilia litakalobeba abiria 155,litaanza safari kwa barabara ya Morocco Gerezani na kwa wiki ya kwanza nauli itakuwa bure kwa masharti watumiaji wawe na kadi
Amesema muda mrefu wameelemewa na mabasi chakavu na machache hali iliyosababisha utoaji wa huduma kulegalega,na sasa wameleta basi la kwanza linalotumia gesi lenye uwezo wa kubeba abiria 150.
Basi hilo ni kati ya mabasi 100 yaliyoagizwa kwa kampuni ya mabasi nchini China,na sasa limeletwa kwa ajili ya majaribio kuona kama limekidhi vigezo walivyokubaliana ikiwamo mafundi na madereva kuzoea mfumo wa ufanyakazi wake.
Akizungumza leo Mei 9,2025 na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa basi hilo wakati wa uzinduzi wa basi hilo,Kindamba amesema wamepokea maelekezo ya bosi ya kuleta mabasi ya kisasa na wametekeleza.
"Kiutaratibu ni lazima utengeneze moja au mawili kisha uyaharibu kulingana na jiografia,mana hutengenezwa kwa kadri ya mazingira ya nchi tofauti.Tukishalijaribu hili watu walipande walikosoe,madereva wetu waliendeshe walikosoe.
"Ili mengine 99 yatakapokuja makosa yale yawe yamerekebishwa,hatukutana kutengeneza yote 100 alafu unakuta yanamakosa hasara yake itakuwa kubwa sana.Huu ni mwanzo tu,tunajua tumepia changamoto nyingi,wananchi wetu wamekata tamaa,wameumia,wameibiwa lakini baada ya dhiki imekuja faraja,Rais Samia Suluhu Hassan amewasikia na ametimiza,"amesema Kandamba.
Amesema litakuwa na internet,kuchaji simu na AC,na kwamba yatakapowasili mengine 99 yatagawanywa kwenye madaraja mbalimbali kwa nauli tofauti ili kujiendesha kibiashara.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED