RIPOTI ya Tathimini ya namna redio zilivyoripoti uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, imebaini kuwa sauti za wanawake wengi hazikusikika kwenye vyombo vya habari kutokana na hofu ya kuharibu mahusiano na wenza au waume zao.
Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo uliohusisha redio 35 za mikoa, kijamii na kitaifa yaliyohusisha habari 990, Mtafiti Mkuu kutoka Shule ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC), Dk. Malima Zacharia, asema vyombo vya habari ambavyo vilitoa nafasi ndogo kwa wanawake vilivyoulizwa walisema ni kwasababu wengi walihofia mahusiano yao.
“Tuliwauliza waandishi kwanini wanawake hawakupewa nafasi ya kutoa mtazamo wao, walisema wanawake wengi wanaogopa kuongea kwneye vyombo vya habari, lakini wanahofia wataonekana vipi na waume zao, hivyo wachache ambao ni ‘single mother’ ndio walikuwa tayari kuongea,”amesema.
Katika utafiti huo asilimia 62 ya vyombo vyote 35 havikuwa na vyanzo wanawake kwenye habari zao, asilimia 23 walikuwa na mwanamke mmoja , asilimia 15 wanawake wawili na kuendelea,”amesema Dk. Malima.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED