Makamu Mwenyekiti wa CCM Stephen Wasira akizungumza na wana CCM leo Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Stephen Wasira amesema umasikini unaweza kuondoshwa kama watu wa vijijini watapate njia ya uwekezaji, akishairi kwamba Progaramu ya Jenga Kesho Bora (BBT) ifike kila mkoa na kuwahusisha wanakijiji badala ya vijana wasomi pekee ili iwasaidie kubadilisha maisha yao.
Akizungumza na wana CCM leo wilayani Chamwino mkoani Dodoma, Wasira amesema baada ya uchaguzi wataangalia namna ya kuboresha ilani inayokuja kwa kutilia mkazo zaidi uzalishaji hasa kwa watu wa vijijini ili kupambana na umasikini.
"Umwagiliaji ni lazima usambazwe na kwakweli nimpongeze sana Rais Samia mimi nilikuwa Waziri wa Kilimo tatizo ambalo lilitukabili katika umwagiliaji ni kutokuwa na mfumo maalumu wa usimamizi wa suala hilo, kama huna hela humwagilii, utamwagilia na mvua tu kwasababu miundombinu ya umwagiliani ni gharama," amesema Wasira.
1 Ametolea mfano Vietnam akisema kutokana na kutumia mfumo wa umwagiliaji sasa ni wazalishaji wakubwa wa mazao ya kilimo kuliko nchi yoyote, akisema ukiwekwa mfumo huo Dodoma italeta mabadiliko kwasababu mvua za eneo hilo hazitabiriki.
"Sasa mkifanya umwagiaji kitu kinaichoitwa njaa na umasikini vitaisha, kwahiyo iangaliwe uwezekano wa kutumia maji ya mvua kutengeneza mabwawa ya kufanya umwagiliaji ili watu inapowezekana walime kwa kutumia trekta badaka ya jembe la mkono ambalo ni shingo ya umasikini.
"Jembe la mkono kwa sasa kwa vijana ni tatizo, na watu tusiwategemee sana kulima kwa jembe la mkoni. Na hiki kitu katika ilani inayokuja tutatazama uwezekano wa kuweka mfumo matrekata ya kutoa huduma ili wakulima wawe wanatumia na kurudisha kwa kulipia," amesma Wasira. 2