Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu akiwa katika Gereza la Ukonga amegoma kuendelea na kesi ya tuhuma za kusambaza taarifa za uongo mtandaoni kwa njia ya mtandao 'video conference'.
Lissu amegoma baada ya kupelekewa taarifa na askari Magereza kwamba anatakiwa afike katika chumba cha Video cha gereza hilo kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa kesi yake, na kudai kuwa hawezi kusikiliza kwa 'Visual'.
Mwenyekiti huyo aligoma kutokea mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Geofrey Mhini wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam aliyekuwa akiendesha kesi hiyo kwa njia ya mtandao.
Ilidaiwa kuwa Aprili 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam mshtakiwa Lissu akiwa na lengo la kulangai umma alichapisha taarifa hizo kupitia mtandao wa YouTube ambapo maneno hayo yalisomeka ' Uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka jana , wagombea wa CHADEMA walienguliwa kwa melekezo ya Rais.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED