Kesi ya tuhuma za kusambaza taarifa za uongo inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ilishindwa kuendelea kwa njia ya mtandao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuanzia saa 3:15 hasi 3:59 asubuhi baada ya mitambo kusuasua.
Vijana wa Mahakama wa masuala ya Tehema walihaingaika kwa muda kwa ajili ya kuwaunganisha kwenye mtandao Mawakili wa Serikali, Gereza la Ukonga alipokuwa Lissu na Hakimu Mkazi Mwandamizi Geofrey Mhini pamoja na mawakili wa utetezi ili waweze kusomana.
Hali iliendelea kudumu kwa dakika kadhaa, Hakimu Mhini alisema hawezi kuendelea na kesi kama hajapata uthibitisho kutoka Magereza kama Lissu yupo huku akiendelea kuwaita mawakili wa Serikali katika kipaza sauti kama wanamsiki huko walipo kwa sababu na wao hawakuwepo mahakamani.
Ilipofika saa 3:24 asubuhi Hakimu Mhini alianza kwa kuita tena ili apate uthibitisho kama Lissu yupo mahakamani na pia kama mawakili wa Serikali wanamsikia, askari wa Jeshi la Magereza aliyeonekana kutoka Ukonga alimuomba hakimu kama dakika mbili wammlete, kwa hiyo aliomba Mahakama ivumilie kidogo.
Baada ya kauli hiyo, baadhi ya watu wakaanza kunong'ona kwa sauti ndipo Hakimu Mhini alipowaeleza kwamba waache kelele na ilipofika saa 3:33 asubuhi hakimu aliwaita tena askari Magereza kama wapo tayari .
Ndipo mmoja wa Mawakili wa Lissu kati ya mawakili 25, Mpare Mpoki alimueleza hakimu kwamba wanapoteza muda wakati vitabu vipo yaani (CPA). "Kama ripoti ya kiufundi ipo basi nipate taarifa nifanye uamuzi,"Amesema Hakimu Mhini
Kijana mmoja wa Tehama wa Mahakama akamueleza hakimu kwamba tayari wameshawasiliana nao. Saa 3:45 asubuhi Magereza wakauganishwa, ambapo Hakimu Mhini alisema anatoa dakika 10 tu zikipita basi atafanya uamuzi.
"Haya Magereza mnanisikia, mawakili.wa Serikali mnanisikia? Mpo tayari? Ndiyo naona mtandao unasumbua,"amesema Hakimu
"Sisi tupo tayari kuendelea kwa wote sababu wote walikuwa wanajua tarehe ya kesi," amedai Wakili Mpoki
Hakimu Mhini alimjibu kwanza hawezi kuendelea hadi awapate pande zote mbili na ilipofika saa 3:59 asubuhi Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga aliieleza Mahakama kuwa wapo tayari kuendelea na askari Magereza amedai kwamba walipomfikishia taarifa Lissu amedai kwamba hawezi kuendelea kwa njia ya mtandao.
Ilidaiwa kuwa Aprili 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam mshtakiwa Lissu akiwa na lengo la kulangai umma alichapisha taarifa hizo kupitia mtandao wa YouTube ambapo maneno hayo yalisomeka ' Uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka jana , wagombea wa Chadema walienguliwa kwa melekezo ya Rais.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED