Ujumbe wa Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) ukiongozwa na Katibu Mkuu wake, Zurab Pololikashvili, umefanya ziara ya utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha leo Aprili 24, 2025, ikiwa ni sehemu ya shughuli za pembezoni mwa Jukwaa la Pili la Kimataifa la Utalii wa Vyakula kwa Kanda ya Afrika linaloendelea jijini Arusha.
Katika ziara hiyo, ujumbe huo ulitembelea maporomoko ya maji ya Tululusia, mojawapo ya vivutio vya kipekee vilivyopo ndani ya hifadhi hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Dk. Pindi Chana, aliongozana na ujumbe huo pamoja na baadhi ya Watendaji kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), wakielezea utayari wa Tanzania kuendeleza na kukuza utalii wa kiikolojia na kitamaduni unaozingatia uendelevu.
Ziara hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha utalii barani Afrika na kutangaza vivutio vya kipekee vya Tanzania katika jukwaa la kimataifa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED