Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira amesema mtaji wa chama hicho ni watu ambao ndio wanawapigia kura na kuwaweka madarakani kutokana na mambo mengi ya kimaendeleo ambayo CCM imeyafanya tangu Taifa lipate Uhuru.
Pia amesema CCM imeendelea kuwa madarakani kwasababu watu wanawakubali, huku akisisitiza viongozi kusikiliza na kufanya vikao vinavyo na kuzungumza kuhusu kuleta maendeleo ya jamii.
Wasira ameyasema hayo leo katika jimbo la Kibakwe wilayani Kongwa, mkoani Dodoma, ambako yuko katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi 2020-25, pamoja na kukagua miradi ya maendeleo.
"CCM tunaajenda ya kudumu ya kubadili maisha ya watu, tunataka maisha yawe mazuri kila mwaka, ya leo yawe mazuri kuliko jana na ya kesho yawe mazuri kuliko ya leo.
"Sasa wengine wanatuuliza CCM mmekaa sana na sisi tunawauliza tulipotafuta uhuru tuliwaambia tunakaa mpaka lini? Tunamkataba gani na nyinyi maana wanaotuuliza ni wajukuu wa waliotutawala pamoja na vibaraka wao wa ndani," amesema Wasira.
Ameeleza kuwa chama hiko kiko madarakani hadi sasa kwa idhini ya watanzania ambao wako kwa idhini ya Mungu, na kwamba ilimradi wanawaunga mkono hawataki kuulizwa swali kwasababu wanakazi ya kufanya.
"kazi yetu lazima itaendelea na ili kuendemea huko ni lazima CCM tuendelee kuongoza katika kuwaletea wananchi maendeleo," amesema Wasira
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED