Kesi za uchochezi na uhaini zinazomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,Tundu Lissu zitasikilizwa kwa njia ya mtandao,huku link ikisambazwa kwa wanaotaka kujiunga kufanya hivyo.
Aidha,viongozi watano wa CHADEMA wamekamatwa kwa nyakati tofauti wakati wakielekea Mahakama ya Kisutu.
"Nimefika Mahakama ya Kisutu, Lissu hataletwa Mahakamani badala yake kesi hii imeamriwa isikilizwe kwa njia ya mtandao,"ameandika Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA,Godbless Lema kwenye ukurasa wake wa X.
"Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam Inayoketi Kisutu Shauri la Jinai namba 202504102000008606 Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geofrey Mhini.Hii ya uchochezi,"ameandika.
"Tafadhali tumia kiungo (link) kifuatacho virtualcourt.judiciary.go.tz/kisutu kuendelea na shauri kwa njia ya mtandao. Shauri limepagwa kwa usikilizaji wa awali leo 24/04/2025 saa tatu asubuhi,"ameandika.
Aidha, Lema amesema Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam inayoketi Kisutu Shauri la Jinai namba 202504102000008607 Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu mbele ya Hakimu Franco Kiswaga.
"Tafadhali tumia kiungo (link) kifuatacho virtualcourt.judiciary.go.tz/kisutu kuendelea na shauri kwa njia ya mtandao. Shauri limepagwa kwa kutajwa leo 24/04/2025 saa tano asubuhi.Hii ya Uhaini,"ameandika.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED