Bashe atangaza hatua kali kwa Malawi, Afrika Kusini

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:50 PM Apr 23 2025
news
Mtandao
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, ametangaza uamuzi mgumu dhidi ya nchi ya Malawi na Afrika Kusini kwa kuzuia mazao yoyote ya kilimo kuingia nchini kutoka na nchi hizo kukakataa kubadili msimamo wao wa kuruhusu mazao kutoka Tanzania kuingia kwenye nchi zao.

Waziri Bashe ametangaza uamuzi hu leo usiku Aprili 23, 2025, huku akisema msimamo ni kupiga marufuku matunda kama apples na mengine kutoka Afrika Kusini kuingia nchini, hadi watakapoondoa zuio kwa Tanzania.

“Kuanzia usiku huu Aprili 23, 2025, hautaruhusu zao lolote linalotoka Afrika Kusini linalohusiana na kilimo kuingia nchini kwetu, 

“Malawi hadi sasa hawajafuta notisi waliyoitoa dhidi ya Tanzania, Natangaza rasmi ni marufuku kwa mazao yoyote ya kilimo kuingia ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia leo. Kwa nchi zote mbili hasa Malawi hatutaruhusu zao lolote kupita nchini kwetu,”amesema.

Aidha, amesema wakati Malawi inawakatalia wafanyabishara wa Tanzania kupita lakini wao (Malawi) kupitia Shirika la Moja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wananunua mahindi kwa hoja ya njaa, kwahiyo mahindi yote waliyonunua kwa ajili ya kutatua tatizo la njaa kwao hayatoenda Malawi, hatutayapeleka na wala hatutaruhusu WFP kuyapeleka hadi watakapofungua soko.

Waziri Bashe amesema Mei 1, 2025 walikuwa wanaanza kuchukua mbolea kutoka Tanzania kwa ajili ya msimu wa kilimo, hatutaruihusu mbolea yoyote kwenda Malawi.

“Hatua hii haihatarishi usalama wan chi wala usalama wa chakula , hakuna mtanzania atakufa kwa kukosa zabibu ya Afrika Kusini, hakuna mtanzania atakufa kwa kukosa Apple kutoka Afrika Kusini, Tunachukua hatua hii kulinda biashara  yetu,”amesema Bashe.

Aprili 17, mwaka huu, Waziri Bashe alitoa siku saba kwa nchi za Afrika Kusini na Malawi kuondoa zuio la mazao ya Tanzania, vinginevyo hatua kali zitachukuliwa.