Wasira kukagua utekelezaji wa ilani Dodoma

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 07:51 PM Apr 22 2025
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Stephen Wasira.
Picha: Mpigapicha Wetu
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Stephen Wasira.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Stephen Wasira, kesho anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi mkoani Dodoma kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi na kuimaimarisha chama.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma ambayo imetolewa leo April 22, 2025, kupitia ziara hiyo Wasira atazungumza na wana CCM na wananchi katika matukio na shughuli mbalimbali.

Pia taarifa imesema katika ziara hiyo ya siku tano, Wasira atatembelea wilaya zote za mkoa huo ambako pamoja na mengine ataweka mawe ya msingi kwa baadhi ya miradi ya maendeleo.

"Wanachama, wapenzi wa CCM na wananchi wote wanaombwa kujitokeza kwa wingi kumlaki Makamu Mwenyekiti Wasira katika maeneo mbalimbali atakayoyafikia kupitia ziara hii," imesema sehemu ya taarifa hiyo.