G55: Hata waliopinga maridhiano hawakufukuzwa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:16 PM Apr 22 2025
Aliyekuwa Mkurugenzi wa ltifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema
picha: Mpigapicha Wetu
Aliyekuwa Mkurugenzi wa ltifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema

Aliyekuwa Mkurugenzi wa ltifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, ameendelea kulalamikia kile alichokiita ni kuvunjwa kwa misingi ya demokrasia ndani ya chama hicho, akisema kwamba zamani CHADEMA ilikuwa na utamaduni wa kusikiliza hoja hata kama ni za kupingana na uamuzi wa vikao.

Akitolea mfano wa maridhiano kati ya CHADEMA, CCM na Serikali, Mrema amesema kuwa licha ya Baraza Kuu kuamua kushiriki maridhiano hayo mwaka 2022, baadhi ya viongozi wa juu wa chama walipinga waziwazi uamuzi huo bila kuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu.

"Walikuwepo Tundu Lissu (wakati huo Makamu Mwenyekiti Bara, sasa Mwenyekiti Taifa), John Heche (sasa Makamu Mwenyekiti Bara), Godbless Lema na Peter Msigwa. Wote waliendesha harakati za kutaka chama kijitoe kwenye maridhiano, lakini hakuna aliyesema wafukuzwe. Hii ni kwa sababu chama kilijengwa juu ya msingi wa kusikiliza," amesema Mrema.