Mapema leo Aprili 21, 2025 Kardinali Kevin Joseph Farrell, ametangaza kifo cha Baba Mtakatifu Francisko kilichotokea majira ya saa 1:35 asubuhi akiwa na umri wa miaka 88.
Katika taarifa hiyo kutoka Roma iliyotolewa na Camerlengo wa Kanisa Katoliki la Roma na la mitume, Kardinali Farell imeeleza kuwa"Papa alizaliwa katika mji mkuu wa Argentina mnamo tarehe 17 Desemba 1936, mtoto wa wahamiaji wa kutoka Piemonte nchini Italia.
Kardinali Farell amesema Papa Francisko atakumbukwa kwa masuala mengi ikiwa ni pamoja na kuwa Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini na Mjesuit wa Argentina, akitambulika kwa jina lake la ubatizo la Jorge Mario Bergoglio, na ambaye alikuwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires tangu 1998.
Amesema alikuwa ni mashuhuri katika bara zima na mchungaji rahisi na aliyependwa sana katika jimbo lake, ambaye alisafiri katika sehemu mbali na mbali, hata kwa njia ya ya ardhi na Bus.
"Watu wangu ni maskini na mimi ni mmoja wao," alisema wakati mmoja kuelezea chaguo lake la kuishi katika ghorofa na kupika chakula chake cha jioni.
HISTORIA YAKE
Papa Francis alizaliwa katika mji mkuu wa Argentina mnamo tarehe 17 Desemba 1936 ambako baba yake Mario alikuwa mhasibu, aliajiriwa kwenye reli, wakati mama yake, Regina Sivori, familia yenye Watoto watano.
Baada ya kufuzu kama fundi wa kemikali, alichagua njia ya upadre kwa kuingia katika seminari ya jimbo.
Machi 11, 1958, alijiunga na Jumuiya ya Yesu (Wajesuit). Alimaliza masomo yake ya kibinadamu nchini Chile na mwaka wa 1963, aliporudi Argentina, alihitimu katika falsafa katika Chuo cha Mtakatifu José huko Mtakatifu Miguel. Kati ya 1964 na 1965 alikuwa profesa wa fasihi na saikolojia katika Chuo cha Bikira maria msafi wa Roho huko Mtakatifu Fé.
Mwaka 1966 alifundisha masomo yale yale katika Chuo cha Salvador huko Buenos Aires. Kuanzia 1967 hadi 1970 alisoma Taalimungu, na kuhitimu kutoka chuo cha Mtakatifu Yosefu.
DARAJA LA UPADRE
Desemba 13, 1969 alipewa daraja la Upadre na Askofu Mkuu Ramón José Castellano. Aliendelea na maandalizi yake kati ya 1970 na 1971 nchini Hispania, na Aprili 22, 1973 alifunga nadhiri za daima katika shirika la Wajesuit.
Alikiwa Argentina, alihudumu kama Mwalimu wa wanovisi huko Mtakatifu Miguel, profesa katika kitivo cha Taalimungu, mshauri wa Kanda ya Jumuiya ya Yesu na mkuu wa Chuo.
Julai 31, 1973 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Kanda ya Kijesuit nchini Argentina. Miaka sita baadaye alianza tena kazi yake katika uwanja wa chuo kikuu na kati ya 1980 na 1986, alikuwa tena mkuu wa chuo cha Mtakatifu José, na vile vile Padre wa parokia tena huko Mtakatifu Miguel.
Machi 1986 alikwenda Ujerumani kukamilisha shahada yake ya udaktari; kisha wakuu wake wakamtuma kwa chuo cha Mwokozi huko Buenos Aires na kisha kwa katika jiji la Cordoba, kama mkurugenzi wa kiroho na muungamishi. Alikuwa ni Kardinali Quarracino aliyemtaka kama kuwa mshiriki wake wa karibu huko Buenos Aires.
Mei 20, 1992 Yohane Paulo II alimteua kuwa Askofu mkuu wa Auca na msaidizi wa Buenos Aires. Desemba 21, 1993 akawa makamu mkuu kisha Juni 3, 1997 alipopandishwa wadhifa na kuwa askofu mkuu mwandamizi wa Buenos Aires.
Miezi tisa baadaye, baada ya kifo cha Kardinali Quarracino, alimrithi, Februari 28, 1998, kama askofu mkuu wa Argentina, wa kawaida kwa waamini wa nchi ya Mashariki mwa nchi na kansela mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki.
Katika Mkutano wa Baraza la Makardinali Februari 21, 2001, Mtakatifu Yohane Paulo II alimteua kuwa Kardinali, na jina la makao yake Mtakatifu Roberto Bellarmino na Oktoba, 2001 aliteuliwa kuwa naibu mwandishi mkuu katika mkutano mkuu wa kawaida wa 10 wa Sinodi ya Maaskofu, iliyowekwa kwa huduma ya kiaskofu.
UINJILISHAJI
Mwaka 2002 alikataa kuteuliwa kuwa rais wa Baraza la Maaskofu wa Argentina, lakini miaka mitatu baadaye alichaguliwa na kisha kuthibitishwa tena kwa muhula mwingine wa miaka mitatu mwaka 2008.
Wakati huo huo, mwezi wa Aprili 2005, alishiriki katika Baraza la Makardinali la Uchanguzi ambalo lilimchangua Papa Benedikto XVI. Akiwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires- wenyeji milioni tatu, alifikiria juu ya mipango ya kimisionari inayozingatia ushirika na uinjilishaji.
Septemba 2009, alizindua kampeni ya mshikamano wa kitaifa kwa miaka mia mbili ya uhuru wa nchi na kuchaguliwa kuwa Papa wa Roma Machi 13, 2013 na leo hii tarehe Aprili 21, 2025 amefariki dunia akiwa amehudumu nafasi hiyo kwa miaka 12.
Raha ya milele ummpe Eee Bwana, Apumzike kwa amani
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED