KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yussuf Mwenda, amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, wamechukua hatua mbalimbali ikiwamo kufukuza kazi watumishi 15, walioenda kinyume na maadili.
Mwenda, amesema hayo jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya taasisi hiyo, kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita.
Aidha, amesema watumishi wengine sita wameshushwa mshahara; 12 walishushwa vyeo na mshahara huku wengine 22 wakipewa onyo la maandishi.
Wakati huohuo, TRA katika kipindi cha miaka minne imefungua kesi 77 za ukwepaji kodi katika mahakama mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kurejesha kiasi cha kodi kilichopotea.
Amesema, ili kuleta usawa katika ulipaji kodi TRA, imeendelea kupambana na wakwepa kodi kwa kuchukua hatua stahikiza kisheria dhidi yao pamoja na kuendelea kutoa elimu na madhara ya kukwepa kulipa kodi.
“TRA, imeendelea kubaini mianya ya upotevu wa mapato na kuchukua hatua stahiki dhidi ya wahusika, hii imeongeza uwajibikaji na kuongeza mapato ya serikali,” amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED