KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Juma Mwenda amepokea makombe matano kutoka kwa timu za michezo mbalimbali za mamlaka hiyo zilizoshiriki na kushinda mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi za Serikali na Mashirika Binafsi (SHIMMUTA) yaliyohitimishwa Desemba 06.2025.
Akipokea makombe hayo jijini Dar es Salaam katika ofisi za TRA leo Disemba 11,2025 Kamishna Mkuu amezipongeza hizo kushinda na kuwataka kutumia michezo kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari.
Mwenda amesema hivi karibuni Bodi ya Wakurugenzi ya TRA imepitisha sera ya michezo ndani ya TRA ambayo itasimamia michezo na kuongeza hamasa ya kulipa kodi kwa hiari kupitia michezo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED