Makipa wa4 wa kuchukua nafasi ya Ter Stegen Barca

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:59 AM Sep 30 2024
Ter Stegen Barca
Picha:Mtandao
Ter Stegen Barca

BARCELONA bila shaka imekuwa timu isiyo na bahati zaidi barani Ulaya linapokuja suala la majeruhi katika wiki za mwanzo za msimu wa 2024/25.

Wachezaji saba wa kikosi cha kwanza - ikiwa ni pamoja na Gavi, Ronald Araujo na Dani Olmo - wote walitolewa kuelekea mchezo dhidi ya Villarreal Jumapili, na wakati wa ushindi wa mabao 5-1 hatimaye jina lingine liliongezwa kwenye orodha ya majeruhi.

Na ilikuwa muhimu sana wakati huo. Nahodha wa klabu na kipa anayeanza Marc-Andre ter Stegen, alitolewa nje na kile ambacho kimethibitishwa kuwa jeraha la goti litakalomuweka nje hadi mwisho wa msimu.

Hapa tunawaangalia magolikipa wanne ambao wanaweza kuchukua nafasi yake, twende sasa...

 1. Keylor Navas

Je, Keylor Navas ndiye mlinda mlango asiyethaminiwa zaidi katika kizazi chake? Ndiyo, bila shaka.

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Costa Rica amekuwa na kipaji mara kwa mara kila mahali alipokuwa, na bado amebadilishwa mara kwa mara na klabu alizochezea.

Kwanza ilikuwa ya Thibaut Courtois akiwa Real Madrid na kisha, ilikuwa Gianluigi Donnarumma huko Paris Saint-Germain.

Navas sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka PSG baada ya kumalizika kwa mkataba wake msimu wa majira ya joto, na atakuwa mbadala wa bei nafuu.

 2. Wojciech Szczesny

Ndiyo, alistaafu soka mwishoni mwa Agosti, lakini baada ya kuandika "mwili wangu bado unahisi kuwa tayari kwa changamoto" kwenye chapisho la kijamii kuhusu kustaafu kwake, bado kuna maisha katika mbwa mzee.

Na ingawa tunasema 'mbwa mzee', katika miaka ya kipa, akiwa na miaka 34, Wojciech Szczesny si mzee kihivyo.

Kipa huyo hakuonesha dalili zozote za kurudi nyuma katika miaka michache iliyopita, akitoa kiwango cha juu mara kwa mara kwa Juventus na Poland.

Sport imeripoti kwamba Szczesny anafikiria kutoka kustaafu na kuwa kipa chaguo la kwanza la Barca. Hakika anatosha kufanya kazi hiyo.

 3. Guillaume Restes

Guillaume Restes mwenye umri wa miaka 19, anaripotiwa kuwa 'anazingatiwa' kama mbadala wa Ter Stegen wakati wa dirisha la usajili la Januari.

Kinda huyo ndiye kipa chaguo la kwanza kwa sasa katika Klabu ya Toulouse ya Ligue 1, na pia katika kiwango cha Timu ya Taifa ya Ufaransa chini ya umri wa miaka 21, akicheza mechi tano hadi sasa.

Ripoti kutoka Sport inadai kuwa Barcelona watakuwa tayari kulipa ada ya euro milioni 15 pamoja na nyongeza ya euro milioni tano ili kumnasa Restes kwenda Katalunya wakati wa dirisha la usajili la Januari.

Ana uwezo wa kuchukua nafasi ya Ter Stegen kwa muda mfupi na mrefu.

 4. Alvaro Valles

Kipa mwingine ambaye Sport imemtaja kuwaniwa na Barca ni Alvaro Valles, kwani anaweza kuonekana kama chaguo la 'fursa ya soko' kwa 'La Blaugrana' hao.

Kutokana na mzozo wa mkataba, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ameondolewa kwenye kikosi cha kwanza cha 'Las Palmas'.

Kwa matokeo hayo, Las Palmas wanajikuta wamejikita mkiani mwa La Liga. Ambayo si bora.

Kusimama kwa mkataba kunaweza kumaanisha kuwa Barca wataweza kumnasa golikipa huyo kwa ada yenye hati punguzo.