Harmonize amuachia Mungu sakata lake na Ibraah

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:59 AM May 15 2025
Harmonize amuachia Mungu sakata lake na Ibraah
Picha: Mtandao
Harmonize amuachia Mungu sakata lake na Ibraah

Msanii Maarufu wa Bongo Flavor,Harmonize amesema kwasasa anamuachia Mungu kuhusu mgogoro uliopo baina yake na msanii Ibraah.

Aidha,amesema anamuombea kila ka heri huku akikana madai ya kutaka alipwe kutaka Sh.bilioni moja.

Harmonize amesema alimtaka Ibraah akamilishe taratibu kama zinavyoelekeza kwenye mkataba ili apate uhuru wa umiliki kamili wa kazi zake zote.

Harmonize maarufu kama Konde Boy ni Mkurugenzi Mtendaji wa Konde Gang,amesema mkataba ulimtaka kama atajiondoa ili awe na umiliki kamili wa nyimbo zake fedha ziingie kwake (Ibraah) lazima alipe kiasi cha fedha kilichotajwa kwenye mkataba.

Amesema mjataba huo alisaini miaka minne iliyopita na Kampuni ya Konde Music, amesema:

 "Sijui nini kimetokea kwake baadaye akasema nimemdai Sh.bilioni moja,nikiri sijamdai bilioni moja na nisingependa pesa yangu ije kunichafua mwenyewe,nimemsamehe na namtakia kila lakeri,nimekuwa na wasanii wengi na wote wameondoka salama,kikubwa wote tunatafuta riziki."

Kuhusu kuitwa BASATA,amesema hakutegemea kama jambo hilo litafika huko na kwamba menejiment yake ilimwakilisha na kwamba kilichozungumzwa atakifafanua wakati mwingine.

Aidha,amekana madai ya Ibraah kuwa Harmonize alimuita chumbani kwake na kumwambia amtoe kafara mama yake.

"Maneno haya yamesambaa sana na sina la kufanya watu wasiamini,Ila namuachia Mungu na nimemsamehe,hana haja ya kuniomba msamaha bali aongee na Mungu wake wakati ukifika,"amesema.

Hivi karibuni kumekuwa na mvutano miongoni mwa wasanii hao huku kukiwa na kurushiana maneno.