Aweso: EWURA yazipa leseni Loliondo, Utete, MANAWASA

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:47 PM May 09 2025
Waziri wa Maji,Jumaa Aweso.
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri wa Maji,Jumaa Aweso.

Kwa kipindi cha 2024/25, EWURA ilitoa leseni tatu (3) za kutoa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa mamlaka za maji za miji ya Loliondo, Utete na Masasi Nachingwea (MANAWASA). Aidha, EWURA ilifanya tathmini na kuidhinisha bei mpya ya huduma ya maji kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga.

EWURA inalo jukumu, hilo kisheria kupitia sheria ya EWURA, Sura Na. 414, inayoipa nguvu  ya kutoa leseni kwa mamlaka za maji na kusimamia masharti ya utekelezaji wake; kudhibiti ubora na ufanisi wa utoaji huduma; kutathmini na kupitisha bei za huduma ya maji; na kutatua migogoro baina ya mtoa huduma na mteja.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Maji,Jumaa Aweso wakati akiwasilisha bungeni, hotuba mapendekezo ya bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwkaa 2025/26, kuanzia Mei 8-9, 2025.

1