EWURA yaidhinisha mikataba 8 huduma kwa mteja

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:32 PM May 09 2025
 Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira (EWURA) imeidhinisha mikataba 8 ya huduma kwa mteja ya mamlaka za maji za Moshi, Makonde, Ruangwa, Songea, Makambako,KASHWASA, Morogoro na Kahama kati ya Julai 2024 hadi Aprili 2025. Katika kipindi hicho, EWURA ilifanya mapitio ya mipango-biashara ya mamlaka za maji 10 nchini.

Sheria ya EWURA Sura Na. 414,  inaipa EWURA majukumu ya kutoa leseni kwa mamlaka za maji na kusimamia masharti ya utekelezaji wake; kudhibiti ubora na ufanisi wa utoaji huduma; kutathmini na kupitisha bei za huduma ya maji; na kutatua migogoro baina ya mtoa huduma na mteja.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso wakati akiwasilisha bungeni, hotuba mapendekezo ya bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwkaa 2025/26, kuanzia Mei 8-9, 2025.