Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (Tanzania Investment and Special Economic Zones Authority - TISEZA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk. Moses Kusilika, Gilead John Teri ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo iliyoanzishwa kufuatia kutungwa kwa Sheria ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Na. 6 ya Mwaka 2025.
Sheria hiyo imeunganisha majukumu ya kilichokuwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na iliyokuwa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED