Ni yule yule, Lengai Ole Sabaya, unayemjua katika ulingo wa siasa za kaskazini mwa Tanzania, amerejea tena.
Sasa ni rasmi, analitaka Jimbo la Arumeru Magharibi, mkoani Arusha.
Baada ya Ole Sabaya, kuchukua fomu ya kuomba kugombea nafasi ya uongozi katika vyombo vya dola, leo asubuhi saa 4:38 ya Julai 1, 2025, amesema neno moja 'Namuachia Mungu afanye kazi yake"
Ole Sabaya, aliteuliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Julai 28,2018.
Pia, amewahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Arusha na Diwani wa Kata ya Sambasha, Halmashauri ya Arusha.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED