Ubunge Moshi Mjini, ni mpambano wa wafanyabiashara

By Godfrey Mushi , Nipashe
Published at 01:29 PM Jun 30 2025
Juma Raibu, akichukua fomu.
Picha: Mpigapicha Wetu
Juma Raibu, akichukua fomu.

Juma Raibu, mfanyabiashara wa mabasi yaendayo mikoani na mmiliki wa maduka ya vifaa vya Electronic, Izaack Ngowi, wamekoleza vita ya wafanyabiashara wanaotaka Ubunge Jimbo la Moshi Mjini, baada ya Ibrahim Shayo (Ibra Line), kufungua pazia hilo Juni, 28 mwaka huu.

Juma, ambaye ni Meya wa zamani wa Manispaa ya Moshi na Izaack, walifuatana kuchukua fomu hiyo ya kuomba nafasi ya uongozi katika vyombo vya dola, walipotinga Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kichama ya Moshi Mjini, leo Juni 30, 2025.

Pia, Juma aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Kilimanjaro na Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya hiyo.

Licha ya Ibra Line, mwaka 2020 kuongoza kura za maoni Jimbo la Moshi Mjini, mshindi wa pili,ambaye ni Mbunge wa sasa anayemaliza muda wake, Priscus Tarimo, naye ni mfanyabiashara wa hoteli, wamechukua fomu hiyo.