Wananchi wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma wamehamasishwa kutambua huduma muhimu za chanjo katika kuokoa maisha ya mtu mmoja mmoja na Jamii kwa ujumla ili kuwapatia taarifa sahihi za utoaji wa huduma za chanjo hapa Nchini na kuwaomba viongozi waendelee kusaidia kuhamasisha na kuelimisha Jamii kuhusu huduma hiyo katika kupinga magonjwa na kuzuia vifo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa idara ya kinga Wizara ya Afya Dr Otilia Gowele kwenye mafunzo ya uhamasiaha wa chanjo Mkoani Ruvuma yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa mikutano uliopo shule ya Sekondari Maposeni halmashauri ya songea ambao umehudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa halmashauri hiyo.
Naye Kaimu meneja mpango wa Taifa wa chanjo kutoka wizara ya Afya Dr Georgina Joachim kwenye mkutano huo alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao wa kike wenye umri wa kuanzia miaka tisa hadi miaka kumi na minne kupatiwa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa kuwa tatizo hilo kwa sasa ni kubwa nchini huku akiwaomba kupinga mila potofu zinazoenezwa na baadhi ya watu kuwa chanjo hizo zina madhara kiafya jambo ambalo sio la kweli.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED