Tajiri namba tatu duniani, Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Amazon, Jeff Bezos (61), anafunga ndoa na aliyekuwa mwanahabari Lauren Sánchez (55).
Kwa wiki nzima shamrashamra zinafanyika mjini Venice, Italia huku Sánchez akionesha mitindo ya harusi ya mabilionea kwa mavazi ya kuvutia na pete inayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni sita (takribani Sh. bil 15).
Wapenzi hao, ambao wamekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka sita, walichumbiana tangu Mei 2023 na sasa wanapanga wanafunga ndoa kwa tafrija leo hii.
Uhusiano ambao umewavutia watu wengi tangu mwanzo sasa upo tayari kufikia hat
Waalikwa ni takribani watu 200 wakiwamo matajiri, waigizaji na wasanii maarufu.
Tangu walipowasili Venice, Jumatano wiki hii, Sánchez kuelekea harusi yake hadi sasa usiku wa harusi katika kidole chake cha mkono wa kulia, amevaa pete ya almasi ya pinki yenye uzito wa karati 30 ambayo Bezos alimvisha wakati wa uchumba wao mwaka 2023, inakadiriwa kuuzwa kati yakuuzwa kati ya dola milioni tatu hadi nne.
Kidole chake cha kushoto, Sánchez amevaa almasi nyingine kubwa zaidi yenye umbo la mviringo, inakadiria kuwa na angalau karati 45 au zaidi, ambayo thamani yake inazidi dola milioni sita.
Ni mara ya kwanza kuvaa pete hiyo pamoja na pete ya uchumba.
Aliziunganisha pete hizo na bangili ya kahawia yenye herufi mbili "LB" ambazo huenda zinawakilisha jina lake jipya, Lauren Bezos.
Walipowasili kwenye hoteli ya Aman Jumatano, Sánchez alivunja mtindo wa harusi wa kawaida kwa kuvaa mavazi meusi badala ya meupe.
Alivalia miwani ya jua ya thamani ya dola 510. Mji wa Venice, unatarajiwa kunufaika kwa kiasi cha dola bilioni 1.1 kutokana na harusi yenye utata na ya kifahari ya Jeff Bezos na Sánchez, kulingana na Wizara ya Utalii ya Italia.
Wizara hiyo ilisema leo Ijumaa kuwa tukio hilo, ambalo limepingwa vikali na baadhi ya wakazi wa Venice, linaweza kuongeza mapato ya utalii ya jiji hilo kwa karibu asilimia 68.
Harusi hiyo ya siku tatu, inaripotiwa kugharimu hadi dola milioni 55 na imewafanya wamiliki wa hoteli na wafanyabiashara wa Venice kuwa na shughuli nyingi.
Licha ya faida za kiuchumi, waandamanaji wamepinga harusi hiyo ya Bezos, mwanzilishi wa Amazon na mtu wa tatu kwa utajiri duniani na Sánchez, aliyekuwa mtangazaji wa runinga.
Mabango yaliyobebwa yalikuwa na ujumbe kama “Hakuna nafasi kwa Bezos” na bango kutoka Greenpeace lililosomeka: “Kama unaweza kuikodisha Venice, kwa harusi yako, unaweza kulipa kodi zaidi.”
Wageni wa harusi hiyo ni takribani 200, wakiwamo watu maarufu kama Bill Gates, Oprah Winfrey, Leonardo DiCaprio, Tom Brady, pamoja na Kim na Khloe Kardashian.
Mapato ya zaidi ya dola bilioni 1 kutokana na harusi ya Bezos-Sánchez ni sawa na robo ya kile wasanii Taylor Swift na Beyoncé walichochangia katika uchumi wa Marekani kupitia ziara zao za muda mrefu.
Mwaka 2023, Michael Grahn, ambaye alikuwa mchumi mkuu wa Benki ya Danske, alitaja ziara ya Beyoncé ya Renaissance kama sababu ya kupanda kwa bei za hoteli na migahawa huko Stockholm.
Ziara hiyo ilichangia zaidi ya dola bilioni 4.5 katika uchumi wa Marekani, kwa mujibu wa utafiti wa kampuni ya QuestionPro.
Ziara ya Taylor Swift ya Eras, iliyodumu karibu miaka miwili na kuwa na matamasha 152 katika miji 51, ilihitimishwa Desemba iliyopita ikiwa ni ziara iliyopata mapato makubwa zaidi kihistoria.
Athari yake kiuchumi ilikadiriwa kuwa dola bilioni tano kwa Marekani, kulingana na makadirio ya QuestionPro.
Hata hivyo, Shirika la Kusafiri la Marekani linasema athari ya kweli ya kiuchumi huenda ilizidi dola bilioni 10 baada ya kujumlisha matumizi yasiyo ya moja kwa moja.
Mapato ya dola bilioni 1.1 kutoka kwa harusi ya Bezos-Sánchez ni zaidi ya dola bilioni moja ambazo Las Vegas ilipata kutokana na Super Bowl ya 2024.
Italia imewahi kuwa mwenyeji wa harusi nyingine maarufu, ikiwa ni pamoja na harusi ya Kim Kardashian na Kanye West mwaka 2014 huko Florence, na ile ya Amal Alamuddin na George Clooney mjini Venice.
Chanzo: CNN/BUSINESS INSIDER
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED