Wakili Peter Madeleka akizungumza na wateja wake waliopata hasara kutokana na kuanguka kwa jengo la ghorofa la Kariakoo, katika viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Divisheni ya Ardhi.
Kesi ya ardhi namba 70 ya mwaka 2025, inayohusiana na kuanguka kwa jengo hilo, imetajwa tena katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Divisheni ya Ardhi.
Wadai katika kesi hiyo ni wafanyabiashara waliokuwa wakifanya shughuli zao katika jengo la ghorofa lililopo eneo la Agiluo, Kariakoo, jijini Dar es Salaam. Mnamo mwezi Novemba mwaka 2024, jengo hilo lilianguka na kusababisha maafa na hasara kubwa kwa wafanyabiashara hao.
Kesi hiyo inasikilizwa mbele ya Mheshimiwa Jaji Abiyaji Muhammadi, ambapo wadai wakuu ni Kanari, Stari Swai na wenzao 49. Washtakiwa katika kesi hiyo ni Zainabu Ismail, Awazi Ashuru, Leo Ndera, Leo Nadi, Ndete na wengine.
Wadai wanadai kupata hasara kubwa kutokana na uzembe wa wamiliki wa jengo hilo na hivyo wanaiomba Mahakama iwape fidia ya zaidi ya shilingi bilioni 40.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED