Makonda sasa rasmi vita na Gambo Ubunge Arusha

By Godfrey Mushi , Nipashe
Published at 04:58 PM Jun 28 2025
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda
PICHA: MPIGAPICHA WETU
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda

Yaliyotabiriwa yametimia. Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amechukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Arusha Mjini (CCM).

Makonda amekabidhiwa mchana leo, Juni 28, 2025, fomu hiyo na Katibu wa CCM, Wilaya ya Arusha, Timothy Sanga. Mei 20, 2025, Makonda aliboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kwa kujiandikisha upya kwenye Kituo cha Hospitali ya AICC, Mtaa wa Mahakama, Kata ya Sekei, Jijini Arusha.

Juni 23, 2025, Rais Samia alifanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa na Makonda hakuwapo katika uteuzi huo, jambo ambalo liliashiria anajitosa katika kinyang’anyiro hicho.