Rais Ndayishimiye ataka Mwekezaji Intracom kuwa balozi wa uwekezaji Tanzania

By Renatha Msungu , Nipashe
Published at 08:50 AM Jun 29 2025
Rais Dk Samia Suluhu akiwa na Rais wa Burundi katika uzinduzi wa kiwanda
PICHA: RENATHA MSUNGU
Rais Dk Samia Suluhu akiwa na Rais wa Burundi katika uzinduzi wa kiwanda

RAIS wa Burundi,Meja Jenerali,Evarist Ndaishmiye amemtaka mwekezaji wa Kiwanda cha Itracom,kuwa Balozi mzuri wa Burundi nchini Tanzania,katika masuala ya uwekezaji mbalimbali.

Ndaishmiye amesema hayo leo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi rasmi wa kiwanda cha mbolea cha Itracom kilichozinduliwa rasmi leo jijini Dodoma na Rais DK Samia Suluhu Hassan
katika hafla iliohudhuriwa na viongozi kutoka nchi jirani.

Amesema muwekezaji huyo anapaswa kuiwakilisha vema nchi ya Burundi katika uwekezaji nchini Tanzania ili kuzidi kudumisha ushirikiano uliokuwepo tokea awali.

"Nampongeza sana Rais Samia kwa kukubali uwekezaji huu ufanyike Tanzania,hii imezidi kuimarisha ushirikiano wetu katika fursa za maendeleo kwa mataifa haya,"amesema Ndaishmiye.

Aidha amesema uwekezaji huo unadhirisha ule usemi wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ya kuwa Waburundi sio wakimbizi ni wahamiaji.na leo hii tunakuja Tanzania kama wawekezaji.

Amefafanua zaidi ya kuwa uwepo wa kiwanda hicho kunazidi kufungua fursa mbalimbali za maendeleo baina ya mataifa hayo Jambo ambalo litazidi kukuza uchumi wa nchi zote mbili.

Amesema pia uwepo wa kiwanda hicho utasaidia kuongeza uzalishaji lakini pia usalama wa chakula utazidi kuimarika ikiwemo kuzidi kuchochea kilimo kwa wakulima.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Itracom Nduwimana Nazaire amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani milioni moja za mbolea kwa mwaka,huku akisisitiza kiwanda hiko kimetengeneza ajira zaidi ya 3,000.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kushawishi wawekezaji kuja kuwekeza mkoani Dodoma ili kuzidi kutnua wigo wa uwekezaji.