Boka kurusha karata Kigamboni

By Pilly Kigome , Nipashe
Published at 10:23 AM Jun 29 2025
Boka kurusha karata Kigamboni
PICHA: PILLY KIGOME
Boka kurusha karata Kigamboni

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Dar es Salaam Abuubakari Ally ( Boka) amejiingiza kwenye kinyang'anyiro cha kuchuana kugombea Ubunge Jimbo la Kigamboni.

Boka ambae pia mtaalamu wa sekta ya afya na mdau wa michezo nchini amefika katika Ofisi za Chama hicho Wilaya Kigamboni na kuchukua fomu ya kinyang'anyiro hicho aliyokabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya hiyo Stanley Mkandawile. 

Boka anaingia katika kinyang'anyiro hicho kupambana na wengine waliochukua fomu akiwemo Ally Mandai,  Injinia Hersi Said na Dokta Henjewele.

Jimbo liko huru baada ya mbunge wa awali Dk.Faustine Ndugulile kufariki dunia na kanuni za uchaguzi kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mdogo kutokana na muda mchache uliobaki kuufikia uchaguzi mkuu.