Prof. Kumburu, Priscus Tarimo katika vita ya siasa

By Godfrey Mushi , Nipashe
Published at 03:30 PM Jun 29 2025
Prof. Neema Penance Kumburu
PICHA: GODFREY MUSHI
Prof. Neema Penance Kumburu

MHADHIRI Mwandamizi wa Kitivo cha Biashara na Sayansi za Mawasiliano cha Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Prof. Neema Penance Kumburu, amejitosa kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kugombea Ubunge, Jimbo la Moshi Mjini.

Mbali na kuomba kuteuliwa kugombea Jimbo la Moshi Mjini, pia Kumburu amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum, akiwakilisha Vyuo Vikuu Nchini.

Mbunge wa Moshi Mjini, anayemaliza muda wake, Priscus Tarimo, leo Juni 29,2025, amechukua fomu ya kuwania Ubunge kwa kipindi cha pili katika jimbo hilo. Tarimo amechukua fomu hiyo majira ya saa 6 mchana katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya kichama ya Moshi Mjini.