TRA yawakumbusha wafanyabiashara kutunza taarifa za biashara

By Shaban Njia , Nipashe
Published at 03:21 PM Jun 29 2025
Ofisa Msimamizi wa Kodi Mkoa wa kikodi kKahama, Jaliwa Wilison, akitoa elimu juu ya usajili wa vyombo vya moto kwa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's)
Picha: Shaban Njia
Ofisa Msimamizi wa Kodi Mkoa wa kikodi kKahama, Jaliwa Wilison, akitoa elimu juu ya usajili wa vyombo vya moto kwa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's)

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa kikodi Kahama, umewakumbusha wafanyabiashara wa kubwa na wa kati kutunza taarifa za bidhaa wanazonunua na kuuliza, ili kuondoa malalamiko yasiyokuwa na tija wakati wa ukadiriaji wa kodi.

Ofisa Msimamizi wa Kodi Mkoa wa kikodi Kahama, Jaliwa Wilison ameyabainisha haya leo, wakati akitoa elimu juu ya usajili wa vyombo vya moto kwa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's) pamoja na washauri wa kodi iliyofanyika katika ukumbi wa manispaa.

Amesema, utunzaji wa taarifa sahihi za ununuzi na uuzaji wa bidhaa kwa wateja inarahisha wakati wa ukadiliaji wa kodi kwani mwaka wa fedha wa TRA, unaonza Januari mpaka Desemba na wale wasikuwa na taarifa hizo ndio wanaibua malalamiko yasiyokuwa na tija.

“Suala hili tumekuwa ukilisema kila tunapowaita kwenye vikao vyetu juu ya utunzaji wa taarifa za ununuzi na mauzo na lengo letu tunataka kuondoa malalamiko ya wafanyabiashara kudai wanaongezewa kodi kila mwaka. Narudia tena leo hii tuhakikishe tunatuza taarifa za biashara tunazofanya," ameongeza Wilison.

Mshauri wa kodi kutoka Ofisi ya Remm Associates, Deus Buyamba amekiri kukosekana kwa taarifa za manunuzi wakati wa upigaji wa hesebu kipindi cha kodi inasababisha wafanyabiashara kulipa kodi kubwa au kidogo na kuiibia serikali mapato yake.

Mshauri wa Kodi kutoka TRA, Esther Paul, akichangia mada wakati wa kikao cha utoaji wa elimu juu ya usajili wa vyombo vya moto kwa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's)