Chama cha ACT Wazalendo kimezindua kampeni ya Operesheni Maji Maji, inayolenga kuwaamsha Watanzania kulinda kura zao kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu wa Idara ya Uenezi wa chama hicho, Shangwe Ayo, alisema: “Ziara hizi ni za kuwaandaa Watanzania kurejesha thamani ya kura zao.”
Kwa mujibu wa Shangwe, kampeni hii ya kitaifa itafanyika kuanzia 1 hadi 15 Julai 2025, ikiongozwa na viongozi wakuu wa chama waliogawanyika katika misafara miwili:
Msafara wa kwanza utaongozwa na Kiongozi wa Chama Dorothy Semu na Makamu Mwenyekiti Bara Isihaka Mchinjita, ukiwa na ratiba ya kutembelea mikoa ya kaskazini na kati.
Msafara wa pili utaongozwa na Kiongozi Mstaafu Zitto Kabwe pamoja na Naibu Katibu Mkuu Bara Ester Akoth Thomas, wakitembelea mikoa ya kusini na magharibi.
Ziara hizi zitahusisha mikutano ya hadhara pamoja na vikao vya ndani na viongozi wa majimbo, kata na wagombea wa ubunge na udiwani.
Kaulimbiu ya kampeni ni: #LindaKura #MuhuniHasusiwi
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED