Wanawake watia mguu Ubunge Moshi Vijijini, Vunjo, Same Mashariki

By Godfrey Mushi , Nipashe
Published at 04:18 PM Jun 28 2025
Gloria Novatus Mushi, Ofisa Rasilimali Watu (HR) wa zamani wa Kampuni ya The Guardian Limited, akisaini kitabu baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge, Jimbo la Moshi Vijijini.
PICHA: MPIGAPICHA WETU
Gloria Novatus Mushi, Ofisa Rasilimali Watu (HR) wa zamani wa Kampuni ya The Guardian Limited, akisaini kitabu baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge, Jimbo la Moshi Vijijini.

Ofisa Rasilimali Watu wa zamani (HR) wa Kampuni ya The Guardian Limited, Gloria Novatus Mushi, ni miongoni mwa wanawake waliojitokeza leo kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge katika Jimbo la Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.

Aidha, Anne Kilango Malecela, naye amechukua fomu kwa mara nyingine kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge katika Jimbo la Same Mashariki. Huku, kada mwingine wa CCM, Lucy Mrema, akichukua pia fomu hiyo akiomba ridhaa ya CCM kuteuliwa kupeperusha bendera Jimbo la Vunjo.

Wengine ni Miriamu Mjema, aliyechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge katika Jimbo la Same Mashariki.