MAKADA tisa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoani Kilimanjaro, wamefungua pazia la uchukuaji wa fomu za kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge katika majimbo manne ya uchaguzi.
Watia nia hao, walichukua fomu hiyo leo, Juni 28,2025, saa 2:00 asubuhi katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi Moshi Mjini, Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Moshi Vijijini na Wilaya ya Hai.
Jimbo la Moshi Mjini, mfanyabiashara, Ibrahim Shayo (Ibra Line), alikuwa wa kwanza kuchukua fomu ya Ubunge katika Jimbo la Moshi Mjini, huku Jimbo la Vunjo, mfanyabiashara, Enock Koola na Yuvenal Shirima, wakizindua zoezi hilo.
Katika Wilaya ya Hai, Fuya Kimbita, ndiye aliyeongoza uchukuaji huo wa fomu, baada ya kutinga ofisi hizo saa 2:00. Wakati, Jimbo la Moshi Vijijini, waliochukua fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Ubunge, ni Abdon Mallya, Deogratius Mushi na Nicodemus Massao. Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela na Miriam Mjema nao walichukua fomu hiyo saa 2:05 asubuhi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED