Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan, amechukua fomu kugombea jimbo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya kuchukua fomu kinondoni amesema amerudi tena Kugombea Kwa lengo la kuwatumikia wananchi wa Jimbo hilo.
"Nimechukua fomu kama nitachaguliwa ndani ya chama kuwaongoza wananchi wa jimbo hili basi nitaongoza kwa kufuata utaratibu na kutekeleza ilani chama",amesema.
Azzan aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kuanzia 2005 hadi 2015 kupitia Chama Cha Mapnduzi(CCM) kabla ya kuangushwa na Maulid Mtulia kupitia Chama Cha Wananchi (CUF).
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED