Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Theobald Mworia, ameingia katika orodha ya vigogo wanaoutaka Ubunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
Mworia, amechukua fomu hiyo leo, Juni 30, 2025. katika Ofisi ya CCM, Wilaya ya Kichama ya Moshi Vijijini, akiomba kuteuliwa katika nafasi ya uongozi wa vyombo vya dola.
Vigogo wengine wanaotaka kuchuana na Mbunge anayemaliza muda wake, Prof. Patrick Ndakidemi, wamo wafanyabiashara, wanazuoni na wahandisi, ni Deogratius Mushi, Abdon Mallya na Nicodemus Massao.
Yumo pia, Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), anayemaliza muda wake, Felister Njau.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED