Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amewakosoa baadhi ya viongozi wa Serikali wanaoibuka na kusema kero za wananchi zimeisha kwa kile alichodai huo ni uongo kero za wananchi haziishi bali hupungua.
Akizungumza jana Juni 30, 2025 kwenye hafla ya kumuapisha Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jubilete Win Lauwo aliyeteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Juni 23, 2025 amesema viongozi wana wajibu mkubwa wa kutatua kero zinazowakabili wananchi, migogoro ya ardhi na migogoro ya kiongozi baina ya viongozi.
"Kero za wananchi ni kitu muhimu sana. Kero haziishi bali zinapungua atakayekwambia kero za wananchi zimeisha ni muongo, kwahiyo ukifanikiwa hili changamoto hii itaibuka, migogoro ya ardhi haiwezi kuisha bali inadhibitiwa na kupunguzwa, kwahiyo kiongozi hodari ni yule anayedhibiti migogoro na kushughulikia kero za wananchi wake,” alisema Mtanda.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jubilete Win Lauwo alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini kuanzia nafasi ya Katibu Tawala huku akiahidi kwenda kuyaishi maelekezo ya Mkuu wa Mkoa, Said Mtanda.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED