TAMSTOA: Tozo mpya ya viwanda itaathiri usafirishaji na biashara

By Grace Gurisha , Nipashe
Published at 11:36 AM Jun 18 2025
Mwenyekiti wa Chama hicho, Chuki Shabani.
Picha: Grace Gurisha
Mwenyekiti wa Chama hicho, Chuki Shabani.

Chama cha Wamiliki wa Malori wa Kati na Wadogo nchini (TAMSTOA), kimesema uanzishwaji wa tozo mpya ya maendeleo ya viwanda kwa kiwango cha asilimia 10 kwa malori itaathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya usafirishaji, biashara ndogo na kati.

Aidha, kimesema wanachama hawajaridhika na ongezeko hilo kwa sababu litalazimisha kampuni kuongeza bei za usafirishaji, gharama ambazo zitahamishiwa kwa mlaji wa mwisho.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Chuki Shabani jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ongezeko hilo kwa kufanyiwa marekebisho kwenye sheria ya Kudhibiti Uingizwaji wa Bidhaa nchini.

"Athari kwa biashara ndoo na kati hutegemea usafiri wa Malori, hivyo ongezeko hili litapunguza faida na uwezo wa kukuza biashara, kampuni ndogo kushindwa kushindana na kuongeza kwa bei za bidhaa," amesema Shabani 

Pia, amesema athari zingine ni wawekezajinwapya kukwepa sekta ya usafirishaji, biashara ndogo kupungua na ipo hatari ya kupungua kwa muda mrefu kutokana na kufa kwa biashara sanjari na wawekezaji kukwepa sekta.

"Ongezeko la asilimia 10 la kodi kwa malori linaweza kudhoofisha sekta ya usafirishaji.Tafiti na ripoti mbalimbali za kitaalamu zimebainisha athari na umuhimu wa mazingira bora ya kodi, tunaomba tukae tuzungumze kama wanatafuta kodi basi waangalie sehemu nyingine," amesema 

Mwenyekiti huyo, ametoa mfano kwamba Scania la mwaka 2013 litaongezewa Sh milioni 4.25 na la mwaka 2018 litaongezewa Sh milioni 10.45 kwa mwaka, hiyo ni gharama kubwa kwa mmiliki mmoja na ikiwa kmapuni ina malori 10 ongezeko linaweza kufikia Sh milioni 100 kwa mwaka.

.