Aliyekuwa Katibu wa NCCR Wilaya Rungwe, Bwana Benard Mwamenywa amejiunga na ACT Wazalendo leo Julai 05, 2025.
Mwemenywa amesajiliwa kidigitali katika cham hicho na Zitto Kabwe; ambaye ni Kiongozi wa Zamani wa ACT Wazalendo.
Tukio hilo limefanyika mara baada ya kumalizika kwa kikao cha ndani cha chama hicho kilichofanyika katika Jimbo la Rungwe, mkoani Mbeya.
Akizungumza mara baada ya usajili huo, Zitto Kabwe amesema hatua hiyo inaonesha mvuto wa ACT Wazalendo unaendelea kuongezeka, huku viongozi kutoka vyama vingine wakijiunga kwa imani ya dhati katika sera na mwelekeo wa chama hicho.
Kwa upande wake, Bernard Mwamenywa amesema amejiunga na ACT Wazalendo kwa sababu ya misimamo imara ya chama hicho katika kupigania haki, maendeleo na uwajibikaji wa Serikali kwa wananchi.
Hivi karibuni wanachama na viongozi wa vyama mbalimbali wamekuwa wakijiunga na ACT Wazalendo. Hii ni ishara nyingine ya kuimarika chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED