Israel yamuua kiongozi wa Hamas na wengine 35

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 03:03 PM Mar 23 2025
Mhusika mkuu wa Hamas Salah al-Bardaweel, aliyeuawa huko Khan Younis Gaza
Picha: Mtandao
Mhusika mkuu wa Hamas Salah al-Bardaweel, aliyeuawa huko Khan Younis Gaza

JESHI la Israel, linaendelea na mashambulizi katika Ukanda wa Gaza na kuuwa takriban watu 35 katika uvamizi wa kabla ya alfajiri, ikiwa ni pamoja na ofisa mkuu wa Hamas Salah al-Bardawil na mke wake waliokuwa wamelala kwenye hema.

Imeelezwa kuwa shambulizi la anga la Israel lilitekelezwa katika mji wa kusini wa Khan Younis huko Gaza, baada ya jeshi hilo kuanza tena mashambulizi makubwa dhidi ya Gaza siku ya Jumanne, likiilaumu Hamas na kuacha makubaliano ya kusitisha mapigano.

Pia imeelezwa kuwa Hamas imekanusha shutuma hizo za Israel na kuishutumu kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yalitiwa saini na kuratibiwa na Qatar, Misri na Marekani.

Wizara ya Afya ya Gaza, imesema Wapalestina 50,021 wamethibitishwa kufariki na wengine 113,274 kujeruhiwa katika vita vya Israel dhidi ya Gaza.

Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Serikali ya Gaza imesasisha idadi ya waliofariki kuwa zaidi ya 61,700, ikisema maelfu ya Wapalestina waliotoweka chini ya vifusi wanakisiwa kuwa wamekufa.

BBC