MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na atu wenye ulemavu, amekabidhi kombati 100, kwa Itifaki ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini.
Kombati hizo zimekabidhiwa leo, Machi 25, 2025 na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Samweli Jackson, kwa niaba ya Mbunge Katambi.
Samweli amesema vijana hao walimwomba Mbunge Katambi awapatie kombati hizo, kwa ajili ya shughuli za kichama na kwamba leo amezikabidhi rasmi, zenye thamani ya Sh. milioni 3.5.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Abdulaziz Sakala, amemshukuru Mbunge Katambi kwa kutekeleza ombi lao, huku wakiahidi kuendelea kushirikiana naye katika shughuli za kichama, na hata kukipatia ushindi chama kwenye uchaguzi mkuu 2025, kwa kuchagua madiwani, wabunge na rais.CCM
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED