Mbunge wa Soy ambaye ni mwanachama wa Chama cha Muungano wa Kidemokrasia cha Rais William Ruto (UDA) David Kiplagat, amedai kuwa amepokea vitisho vya kutisha vya kuuawa, jambo lililosababisha hofu kubwa kuhusu usalama wake.
Imeelezwa kuwa ufichuzi huo umeibua hofu kuhusu uwezekano wa ongezeko la vitisho vinavyolenga viongozi wa kisiasa nchini Kenya.
Mbunge huyo ameeleza leo kuwa kuwa barua za ajabu ziliachwa nje ya nyumba yake iliyoko Uasin Gishu, zikimwonya dhidi ya kutotoka nje ya makazi yake.
“Makini! Makini! Unapiga kelele sana. Endelea hivyo, na tutahakikisha hautasema tena. Hii si mjadala, hili ni onyo la mwisho,” imesomeka moja ya barua za vitisho.
Kufuatia vitisho hivyo, wakazi wa Soy wamejitokeza barabarani kwa muda wa saa sita wakitaka serikali iimarishe usalama wa mbunge wao.
Wakazi hao pia wameitaka idara ya usalama kuchunguza tukio hilo na kuwachukulia hatua wahusika. “Hatutakubali mbunge wetu auawe. Tunataka Mheshimiwa apewe ulinzi wa kutosha”.
“Ikiwa hakuna usalama, basi sisi wenyewe tutakuwa walinzi wake,” mkazi mmoja aliambia Citizen TV. “Tumeamka na tukio la kushtua. Kuna mtu anasambaza barua za vitisho kwa mbunge wetu. Hatutakubali hilo,” mkazi mwingine amesema.
Imeelezwa kuwa mbunge huyo, ambaye ni mwanachama wa cha tawala nchini Kenya UDA, tayari ameripoti vitisho hivyo katika Kituo cha Polisi cha Ziwa.
KTN
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED