Basil Lema, Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Kilimanjaro, aliyekumbana na rungu la 'fukuzafukuza' linaloendelea hivi sasa, amesema bado hajapokea barua rasmi zaidi ya kuiona katika mitandao ya kijamii.
Lema, aliyekuwa Mkufunzi Mkuu wa michakato yote ya uchaguzi ndani ya CHADEMA tangu alipojiunga nacho mwaka 2004, amesema anachotaka ni haki ya kusikilizwa ndani ya siku 14 kama katiba ya chama inavyoelekeza, na wala sio kama anaogopa kufukuzwa.
Mei 7 mwaka huu, Katibu wa CHADEMA, Kanda ya Kaskazini, Ndonde Tottinan, alitoa taarifa kwa rasmi ya kusimamishwa kazi Lema kutokana na tuhuma za usaliti.
Kwa mujibu wa Ndonde, hatua hiyo imechukuliwa baada ya Lema, kushukiwa kuwashawishi baadhi ya viongozi wa majimbo, kujiondoa ndani ya CHADEMA na kuhudhuria kikao kilichofanyika Alhamisi iliyopita katika Mji wa Moshi, kwa ajili ya kujiunga na chama kingine cha siasa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED