Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla, amewataka wananchi wasirudie makosa ya awali ya kuchagua upinzani, kwa kuwa chini ya CCM majimbo yametulia na maendeleo yanaonekana.
Akizungumza leo Mei 8, 2025, katika mkutano wa hadhara Ifakara, wilayani Kilombero, mkoani humo, amesema Kilombero aliyokuwa anaijua si ya sasa, kuna mabadiliko makubwa ya maendeleo.
Makalla amesema wanawaahidi walikoishia wanaanzia hapo kusonga mbele katika kuwaletea maendeleo wananchi.
“Tunaamini wananchi wanakichagua CCM kutokana na hali ya amani na utulivu na sisi tunaahidi kimsingi ya amani na utulivu imeasisiwa na CCM na tutahakikisha nchi yetu inaendelea kuwa ya mfano kwa amani na utulivu,” anasema.
Makalla anasema wakati ule alipokuwa akija kulikuwa hakuna daraja wala barabara, wenzao wanaopinga wanashindwa hata kupapasa kwa kiguu kuliona.
“Mtu anakuja inawezekana ni mtalii huwezi kuwadanganya wana Kilombero kuhusu maendeleo,” anasema.
Amesema changamoto hazikosekani na CCM muda wote kimejipambanua wanawajibu wa kutatua changamoto na si kuzikimbia.
Makalla amesema pamoja na changamoto za mafuriko, bado serikali haiwaachi wananchi wa Kilombero, ndio maana kunapotokea matatizo hayo wanamwona Mkuu wa Mkoa pamoja. A Waziri wanawakimbia haraka.
“Changamoto zinazokuja na mafuriko haziletwi na CCM yanatokea nje ya uwezo na serikali inatafuta ufumbuzi. Ufumbuzi ndio huo ambao Mkuu wa Mkoa amesema hapa wataleta fedha kwa ajili ya kukabiliana na mafurikio.
“Watani wetu wanataka yatokee muda wote wanayafurahia. Ninawaomba msimame na CCM, wengine hawana bajeti, hawana dhamana zaidi ya chama tawala, amesema. Makalla amewakumbusha wananchi wa Mlimba na Kilombero kuwa waliwahi kuonja sumu na kazi ya upinzani ni kupinga na wanapenda waendelee kuwa na matatizo.
“Ninauhakika hivi bado mnahamu ya kuwa na wabunge wa upinzani, hakuna kilichofanywa, hawakuwa na nguvu, ninataka tuwaambie tuko imara msirudie makosa hayo yalikuwa majimbo matatu yamepangana walichukua,” amesema.
Makalla amesema majimbo hayo chini ya CCM yametulia kikubwa ni kuwaletea wananchi maendeleo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED