Mawakili 324 nchini, wameanza rasmi mchakato wa kufikia ndoto zao za kujinasua katika madhila ya maisha wanayopitia kwa asilimia kubwa, baada ya kuanzisha ‘Wakili Welfare Mkoba’ ambayo itakusanya Sh. bilioni sita kwa muda wa miaka mitatu ili kuja na benki yao.
Akizungumza jana Jijini Arusha (Mei 6,2025), wakati wa Mkutano Mkuu wa Wakili Welfare Mkoba (WWM), Mwenyekiti wake, Wakili Laetitia Ntagazwa, amesema wazo la kuanzishwa kwa taasisi hiyo, limetokana na wanachama wachache, kuonja madhila ya maisha wanayopitia asilimia kubwa ya mawakili.
WWM kilichozaliwa Disemba 24, 2023, kinaundwa na Mawakili wa Serikali na Mawakili wa kujitegemea.
“Baadhi ya madhila hayo ni pamoja ugonjwa, ajali, kifo, kukosa na kukutana na mikopo yenye riba kubwa kwenye mabenki na taasisi za kifedha. Mawakili kukosa mitaji ya kuanzisha ofisi baada ya kusajiliwa, na baadhi kukosa mitaji ya kuendesha ofisi zao, hata baada ya kuanzisha ofisi hizo za Uwakili.
…Ili kutimiza lengo hilo, kwa miaka mitatu yaani mwaka 2025 hadi 2027, tunatarajia kukusanya shilingi bilioni sita za Kitanzania, ambapo kwa mwaka huu wa 2025, tunapaswa kukusanya bilioni mbili, na hii imeingia kwenye mpango kazi wa mwaka huu.”
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED