Bilioni 28 zatumika miradi ya maji Bunda

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 07:02 PM Mar 06 2025
'Serikali imetoa kiasi cha zaidi ya Sh. bilioni 28 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji'
PICHA:MPIGAPICHA WETU
'Serikali imetoa kiasi cha zaidi ya Sh. bilioni 28 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji'

KATIKA kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, serikali imetoa kiasi cha zaidi ya Sh. bilioni 28 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Bunda, (BUWSSA).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa taasisi za umma kueleza mafanikio ya miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan, yanayoratibiwa na Idara ya Habari-Maelezo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Esther Gilyoma, alisema tangu kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya sita katika uongozi Mamlaka hiyo imepitishiwa miradi ya thamani ya Sh. Milioni 28.1 na Sh.Bilioni 11.89 tayari zimepokelewa na baadhi ya miradi imekamilika na mingine utekelezaji unaendelea.

Amesema, miongoni mwa miradi iliyokamilika ni Mradi wa ujenzi wa chujio la maji Nyabehu – Bunda ambayo umegharimu Sh.Bilioni 10.6 na wananchi 227,446 wananufaika na mradi huo.