MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imesema inaendelea kuweka mazingira rafiki ya kuhamasisha uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa biashara ya gesi asilia iliyogandamizwa (CNG) ikiwa ni hatua muhimu katika kusaidia juhudi za Serikali za kuchochea matumizi ya nishati safi nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Ewura Dr James Andilile wakati wa majadiliano kwenye jopo katika Mkutano wa 11 wa Petroli wa Afrika Mashariki (EAPCE’25) unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo wa siku tatu, ulianza jana na unashirikisha Wadau mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Msuya amesema kuwa moja ya hatua muhimu zilizokwisha kuchukuliwa kuhamasisha uwekezaji ni pamoja na kuondolewa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye miundombinu muhimu ya CNG.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED