Kampuni ya uzalishaji wa vinywaji baridi jamii ya Coca Cola ya Bonite Bottlers Limited (BBL), imesema programu yake endelevu ya uhifadhi wa mazingira na urejeshwaji wa bioanuai kuzunguka Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro, iliyoasisiwa na Hayati Dk. Regnald Mengi, kwa mwaka huu imepanda zaidi ya miti 500.
Akizungumzia zoezi hilo la upandaji miti katika Shule kongwe ya Sekondari ya Ufundi Moshi, Mratibu wa Masoko wa BBL, Leonard Makule, amesema kati ya idadi hiyo, miti 200 iliyooteshwa ni ya matunda na miti 300 ni ya kivuli.
"Tunafanya hivi kuunga mkono kauli mbiu ya siku ya mazingira duniani, ambayo huadhimishwa kila Juni 5. Kampuni ya Bonite Bottlers Limited inafanya kila iwezekanalo kuhakikisha tunahifadhi kwa nguvu zote mazingira ya Mlima Kilimanjaro.
...Kupanda miti hatujaanza leo, tangu alipokuwapo mwasisi wa Kampuni yetu, Hayati Dk. Reginald Mengi. Hii ni kutokana na kiu yake kubwa ya kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko tabianchi, ili kuhakikisha uoto wa asili na bioanuai ya Mlima Kilimanjaro , inazidi kuwepo na kuvutia watalii wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED