CHAMA cha Mapinduzi kimelaani tukio la kushambukiwa Katibu Mkuu wa Baraza ka Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Dk.Charles Kitima
CHAMA cha Mapinduzi kimelaani tukio la kushambukiwa Katibu Mkuu wa Baraza ka Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Dk.Charles Kitima.
Aidha,kimesema kimepokea kwa masikitiko taarifa hizo na kwamba si kitendo cha kikatili na kisicho na utu dhidi ya kiongozi wa dini ambaye amejitolea maisha yake kuhudumia jamii kwa upendo na uadilifu.
"CCM inatoa wito kwa vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina na haraka ili kuwabaini na kuwachukulia hatia kali waliohusika na tukio hili,"amesema Katibu Mkuu wa CCM,Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi katika taarifa yake kwa umma.
"CCM inatoa pole kwa Padri Kitima,familia yake,TEC,na waumini wote wa Kanisa Katoliki kwa mshtuko na maumivu yaliyosababishwa na tukio hili,"amesema.
Aidha,amesema CCM inamuombea Padri Kitima uponyaji wa haraka ba kurejea katika majukumu yake ya kiriho na kijamii.
Dk.Nchimbi amesema CCM itaendelea kushirikiana na taasisi zote za dini katika kujenga taufa lenye kulinda na kuendeleza misingI ya amani,umoja wa kitaifa,mshikamano,heshima na linaloheshimu haki za binadamu,"amesisitiza.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED