Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) imekamilisha upembuzi yakinifu kwa ajili ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa katika Jiji la Dodoma (Dodoma Commuter Train).
Ujenzi wa reli hiyo unalenga kuimarisha usafiri katika Jiji la Dodoma kwa kuunganisha jiji hilo na viunga vyake ikiwemo Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Msalato.
“Mheshimiwa Spika, hivi sasa serikali ipo katika hatua za utafutaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa reli hiyo,” amesema
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile, amesema hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum Fatma Toufiq aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kujenga Reli ya kisasa kutoka kituo kikuu cha SGR Dodoma hadi Uwanja wa Ndege Msalato.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED