Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amesema serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kuongeza mapato ya ndani ili kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya bajeti inagharamiwa kwa kutumia mapato ya ndani.
Nchemba, amesema leo bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini Prof. Patrick Ndakidemi, aliyehoji kuwa serikali imejiandaa vipi kukabiliana na mabadiliko ya Sera za baadhi ya nchi tajiri kulisaidia Taifa kukuza uchumi.
“Aidha, kwa kutambua umuhimu wa mahitaji ya kibajeti ikiwemo ugharamiaji wa miradi ya maendeleo, serikali itaendelea kuvutia ushiriki wa sekta binafsi katika ugharamiaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia njia mbadala ikiwemo ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi,” amesema
Amesema hiyo itasaidia kuipunguzia serikali mzigo wa kukopa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kupunguza utegemezi wa kibajeti kutoka kwa Washirika wa Maendeleo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED